Social Icons

Friday, 29 November 2013

MHUBIRI WA KIMATAIFA DR. DANIEL MOSES KULOLA KUZURU MAREKANI MWEZI WA DECEMBA 2013

Pastor na mwinjilisti wa Kimataifa ambaye ndiye mtoto pekee ambaye amerithi huduma na majukumu ya askofu mkuu marehemu   Dr Moses Kulola aitwaye Dr. Daniel Moses Kulola amepata mwaliko wa kuelekea Washington Dc Marekani kwa huduma ya mwezi mmoja na nusu kuanzia 17 Desemba hadi 30 january 2014.
Akieleza juu ya safari hii kubwa kuwa muda mwingi amekuwa akialikwa kwenda marekani lakini kuna mambo mengi yalikuwa yanaingilia kati kuwa kizuizi. Lakini baada ya mazishi ya baba yake ambaye ni baba yetu sote ameona ni vyema kusafiri kwenda katika huduma maana wengi wamekuwa wakimuhitaji katika nchi hiyo iliyojaa mambo mengi.
Dr. Daniel kulola amekuwa ni moja ya wahubiri wachache ambao wamepata neema ya kipekee ya kwenda kuhubiri katika nchi nyingi zilizoendelea kama uingereza, ujerumani, Dernmark na kwingineko kwingi. Na taarifa ambazo tumeendelea kuzifuatilia kwa karibu ni kuwa kwa sasa ndiye mhubiri pekee ambaye ameweza kutunza na kuzifuata nyayo za askofu mkuu marehemu Moses kulola na pia ndiye mwenye kibali kikubwa hasa katika makanisa ya EAGT.
Nikiongea naye anasema amealikwa na kanisa la Bethel kingdom church la washington Dc linaloongozwa na askofu Merchizedek pia ataendelea kuhudumu maeneo mbali mbali pamoja na kanisa la Miracle Life worldwide la jimbo la Texas, pia atafika New York.
pamoja na yote kipindi atakwenda peke yake tofauti na ilivyozoeleka kila anaposafiri huwa anasafiri na mkewe Mercy Daniel katika huduma zake zote akifuata nyayo za baba yake.
alitoa pia dokezo atakapo rudi atafanya uzinduzi wa kitabu cha maisha ya mzee Moses kulola ambacho kwa sasa kimekamilia kwa asilimia kama 97. Kimeandaliwa kama kwa miaka 2 hadi na nusu hivi na msimamizi wa kitabu hicho ni yeye mwenyewe Dr. Daniel kulola.
alimalizia kwa kusema anahitaji maombi ya wana injili wote wawe naye hasa katika kipindi hiki cha mpito pia alisema ataondoka Tanzania 15 Dec na kufika washington Dc 16 Dec na kuanza huduma ambayo itampeleka hadi 30 Jan 2014.
ukipenda maombi na ushauri pia simu yake iko hewani +255 767 749040 na +255 784 749040
 Hapa Dr Kulola akiwa kwenye mikutano tofauti akinena neno la uzima kwa nguvu
m


 
This Blog Developed And maintained By: MITSOLN