Featured Posts
Saturday, 7 December 2013
WASHINGTON DC kwa YESU CHRISTMAS CONFERENCE
ULE WAKATI UMEFIKA,
Siku zilikuwa ni nyingi na sasa muda umefika ambapo ile conference ya kimataifa ya Washington Dc ikihudumiwa na mtumishi wa Mungu Dr. Daniel Moses Kulola imewadia
Taarifa za uhakika mhubiri tayari ataondoka Tanzania siku ya jumapili 15/12/2013 WATU WOTE KARIBUNI SANA MBARIKIWE HASA KIPINDI HIKI CHA KUINGIA MWAKA 2014
Saturday, 30 November 2013
KANALI MSTAAFU MBILIZI KATUTOKA
kanali Shadrack Mbilizi moja wa makanali shupavu wa jeshi la wananchi wa Tanzania amefariki Dunia.
Kwa taarifa ambazo tumezipata kutoka katika vyanzo vyetu vya habari kanali Mbilizi ambaye baada ya kustaafu jeshini mwaka 1988 alirudi kuishi mji mdogo wa Lugeye nje kidogo ya Nyanguge mkoani mwanza alifariki alfajiri ya tarehe 28 Novemba 2013 katika Hosp ya Rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa.
Habari zimeendelea kuripotiwa alikuwa amepatwa na presha ya ghafla akapelekwa kwa matibabu mjini Magu ambako ilionekana anahitaji matibabu zaidi ndipo alihamishiwa Bugando Hosp... baada ya matibabu alitolewa na kukaa katika moja ya familia ya wanawe ili awe karibu na huduma za hosp siku ya kurudi hosp kwa uchunguzi zaidi. Lakini hali yake ilibadilika ghafla na kurudishwa Bugando hosp na kisha kuwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ambako ndiko mauti ilimkuta tarehe 28 Nov alfajiri.
Taarifa kutoka kwenye familia inasema aliagizwa kuzikwa kijeshi pindi ikitokea siku moja hayuko duniani.. baada ya kutoka duniani familia iliweka taratibu pamoja na viongozi wa kijeshi.... Marehemu Kanali Mbilizi hadi anatutoka alikuwa na miaka 90 kwani taarifa inaonyesha alizaliwa 27 machi 1923 na kufariki 28 Nov 2013.
Msiba huu mkubwa unagusa familia kubwa za jijini mwanza ikiwa ni pamoja na familia ya marehemu askofu mkuu Dr. Moses kulola. Marehemu kanali Mbilizi ndiye sanji wa Mzee kulola kwa mwanawe Pastor Dr. Daniel Kulola ambaye ameoa kwake.
Kwenye mambo kama haya huwa hapakosekani na mambo ya kushangaza na kufurahisha pia..Tukio la kuashiria mema lilitamkwa na mwongoza mazishi mch na mwinjilisti wa AIC kiongozi wa kanisa marehemu alikuwa akiabudu alipotaka ibada ya mazishi ifunguliwe ,,, kupitia kwenye microphone alitamka tunamkaribisha askofu Dr. Daniel Kulola aje kutufungulia ibada yetu... watu wote wakasema na iwe hivyo... badaa ya mazishi kila mmoja alimfuta mch huyo na kuanza kumpa hongera na kumwambia ndivyo tunataka... ila Mch Daniel Kulola alionekana kunyamaza kimya tu...kidogo akimwangalia mama yake na yeye kusema mapenzi ya Mungu yanaonekana.
Akizungumza kwa huzuni dr Kulola alisema familia imepoteza kiongozi mzuri na shupavu katika nchi na kifamilia pia. Tutazidi kumkumbuka na kuyaenzi mazuri ya kanali alimalizia kwa kusema hivyo.
Marehemu ameacha watoto hai 13 na wajukuu pia watukuu na mke mmoja.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA MBINGUNI---AMEN
Friday, 29 November 2013
MHUBIRI WA KIMATAIFA DR. DANIEL MOSES KULOLA KUZURU MAREKANI MWEZI WA DECEMBA 2013
Pastor na mwinjilisti wa Kimataifa ambaye ndiye mtoto pekee ambaye amerithi huduma na majukumu ya askofu mkuu marehemu Dr Moses Kulola aitwaye Dr. Daniel Moses Kulola amepata mwaliko wa kuelekea Washington Dc Marekani kwa huduma ya mwezi mmoja na nusu kuanzia 17 Desemba hadi 30 january 2014.
Akieleza juu ya safari hii kubwa kuwa muda mwingi amekuwa akialikwa kwenda marekani lakini kuna mambo mengi yalikuwa yanaingilia kati kuwa kizuizi. Lakini baada ya mazishi ya baba yake ambaye ni baba yetu sote ameona ni vyema kusafiri kwenda katika huduma maana wengi wamekuwa wakimuhitaji katika nchi hiyo iliyojaa mambo mengi.
Dr. Daniel kulola amekuwa ni moja ya wahubiri wachache ambao wamepata neema ya kipekee ya kwenda kuhubiri katika nchi nyingi zilizoendelea kama uingereza, ujerumani, Dernmark na kwingineko kwingi. Na taarifa ambazo tumeendelea kuzifuatilia kwa karibu ni kuwa kwa sasa ndiye mhubiri pekee ambaye ameweza kutunza na kuzifuata nyayo za askofu mkuu marehemu Moses kulola na pia ndiye mwenye kibali kikubwa hasa katika makanisa ya EAGT.
Nikiongea naye anasema amealikwa na kanisa la Bethel kingdom church la washington Dc linaloongozwa na askofu Merchizedek pia ataendelea kuhudumu maeneo mbali mbali pamoja na kanisa la Miracle Life worldwide la jimbo la Texas, pia atafika New York.
pamoja na yote kipindi atakwenda peke yake tofauti na ilivyozoeleka kila anaposafiri huwa anasafiri na mkewe Mercy Daniel katika huduma zake zote akifuata nyayo za baba yake.
alitoa pia dokezo atakapo rudi atafanya uzinduzi wa kitabu cha maisha ya mzee Moses kulola ambacho kwa sasa kimekamilia kwa asilimia kama 97. Kimeandaliwa kama kwa miaka 2 hadi na nusu hivi na msimamizi wa kitabu hicho ni yeye mwenyewe Dr. Daniel kulola.
alimalizia kwa kusema anahitaji maombi ya wana injili wote wawe naye hasa katika kipindi hiki cha mpito pia alisema ataondoka Tanzania 15 Dec na kufika washington Dc 16 Dec na kuanza huduma ambayo itampeleka hadi 30 Jan 2014.
ukipenda maombi na ushauri pia simu yake iko hewani +255 767 749040 na +255 784 749040

Hapa Dr Kulola akiwa kwenye mikutano tofauti akinena neno la uzima kwa nguvu
Friday, 22 November 2013
SEMINA MOTO MOTO - EAGT LUMALA MPYA, JIJINI MWANZA
Kanisa la EAGT Lumala Mpya chini ya mch na mhubiri wa kimataifa Dr. Daniel Kulola limeanza semina ya uamsho mkuu ndani ya ukumbi wa kanisa hilo. Mhubiri katika Semina hiyo ni Mwinjilist Justine Mpogole kutoka Morogoro.
Semina hiyo ikipambwa na vinjonjo vya waimbaji kemkem kama vile Agnes Akrama mama wa kuwekeza kwa Yesu, bila kumsahau Happy Shamawele ambaye wiki iliyopita alikuwa kwenye Huduma jijini Kigali nchini Rwanda. Wengine ni Sarah Emanuel huyu naye ni hatari anaimba kwa utulivu mkuu lakini watu wakibarikiwa sana, Agnes Mpangala ambaye naye wiki iliyopita alikuwa Nairobi nchini Kenya. Hao ni waimbaji mmoja mmoja.
Kwa habari ya Makundi kuna kundi matata kabisa kwanya ya Uinjilisti, Ufunuo na Kwaya inayo kuja kwa kasi sana ya Hot spear singers. Mwitikio umekuwa wa kushangaza kwani watu wamekuwa ni wengi sana sana. Ni ombi letu tu kuwa nafasi bado ipo watu wafike kujilisha neno la Mungu.
Kanisa liko nyuma ya soko jipya la Saba saba Lumala, Mwanza.
Kwa mawasiliano, wasiliana na mch mwenyeji Dr. Daniel Kulola - 0767 749040
Wednesday, 20 November 2013
Mkutano mkubwa wa injili-2013
Mtumishi wa Mungu Rev. Dr. Daniel Moses Kulola akihubiri katika mojawapo ya mikutano iliyofanyika nchini Tanzania